2011
Download Bongo Flava For Promo Only
Hiya Bongo Flava Fans U can Download these Track Listing By CLICK HERE For Promo Only
3.5 Mb Staminah_-_Punch_after_punch.mp3
3.9 Mb Dastamina_(Shettah,_Vedasto,_Chivalo)_ft_Kasim_-_Hunidai_sikudai_Prod_by_Marco_Chali.mp3
3.7 Ben Pol – Namba 1 fan.mp3
3.1 Mb LchroniCle_-_Nakupenda_Wewe.mp3
6.1 Mb a.v.i.d-Make It Better.mp3
3.7 Mb Ommy_G_-_Mtoto_wa_Nyumba_ile.mp3
4.3 Mb Izzo_B_-_Riziwani.mp3
4.9 Mb Solo Thang – Soulmate.mp3
4.6 Mb Nuruel_Ft_Joslin_-_Nyumbani_produced_by_Lamar_FishCrab.
7.7 Mb BATA BOY – JOS MTAMBO Ft. -Babuu Wakitaa, Cowboy, Fid Q, Adam Mchomvu, Rama Dee & Joslin.mp3
3.9 Mb K.sher ft Marlaw – Hamu.mp3
5.2 Mb ALLY KIBA_MAPENZI YANARUN DUNIA_SONG.mp3
6.3 Mb PETER MSECHU FT BELLA – UNANIUMIZA (Produced By Pancho Latino & Hermy B).mp3
3.7 Mb Chibdayo ft Marlaw – Kuwa naye_Produced by Marco Chali.mp3
3.7 Mb Winfrida ft AY – I need you Back_Produced by Marco Chali.mp3
4.3 Mb rudi.mp3
5.2 Mb Here We Go-Wakacha(Prod by Pancho Latino,Mixed n Mastered By Hermy B) .mp3
7.5 Mb BENNY LEE – NIMEKUFANANISHA.mp3
3.3 Mb KAMA IPO MX MASTERD.mp3
9.8 Mb WATEULE VILE VILE EXT VERSION.mp3
6.6 Mb NOORAH – LUGHA GONGANA (Produced By Hermy B) Radio Master.mp3
4.7 Mb Jogoo feat. Maulo & Bela Kombo 1.mp3
3.7 Mb Jaffarai ft Wayre – Mcharuko.mp3
4.5 Mb Mesen_-_Nyamu.mp3
4.2 Mb Young Dee Ft Mataluma, Kitokololo, Chekedaa – Tunapeta.mp3
6.5 Mb Lady_Jay_dee_Ft_Mr_Blue_-_Wangu
11.1 Mb Commando Yosso (I Think I’m PUZA).mp3
4.7 Mb Bwana Misosi Ft Juma Nature & Fid Q – Pilato na Game.mp3
6.3 Mb Nonini ft Chege(TMK) & Lady-Kila Moja (Sound Track To Killer Mmoja Movie) B.mp3
4.3 Mb 01_Godzilla Feat Marco Chali_KINGZILLA_Produced_By_Marco_Chali.mp3
7.3 Mb GOSBY_FEAT_GODZILA_AND_YOUNG_DEE_MABEGI_BILA_NAULI_
3.9 Mb D knob – Mr sahani.mp3
4.4 Mb Adam Mchomvu- Johny.mp3
2.5 Mb 6.7punchlines (6 foot 7 foot bongo version).mp3
2.5 Mb MWANAUME FULL MIX (master).mp3
3.3 Mb kazi za atm – SirLeh feat Noorah & Mwana F.mp3
3.9 Mb JCB FT-FID Q,JAY MOE & CHUMA-UKISIKIA PAAAAHHH.mp3
5.7 Mb Chidi_beenz_Ft_Mzee_yusuf_-_Maashaalah
www.gongamx.com
3.6 Mb Dully_Sykes_-_Bongo_Fleva
www.gongamx.com
5.7 Mb Lord_Cash_-_Network_buzy_
www.gongamx.com
3.7 Mb Belle_9_-_Nilipe_Nisepe
www.gongamx.com
3.6 Mb Nikki_wa_2_ft_Pipi_-_Kiujamaa_-_
www.gongamx.com
3.5 Mb Mr._Chocolate_-_Oyoyo_
3.5 Mb Aneth_Kushaba_-_Siku_Nazo_(www.gongamx.com)
3.9 Mb RAMA DEE_NAJUA .mp3
816.7 Kb CODE RED MARCH MADNESS.mp3
3.9 Mb Jaffarai_Ft_Lady_Jay_dee_-_Sio_Kweli.mp3
www.gongamx.com
3.4 Mb MwanaFA_-_Unanijua_unanisikia_(CLUB_EDIT)_Produced_By_Hermy_B.mp3
2.4 Mb One_-_40_barz_Bonus_Track_The_Element_Mixtape
7.3 Mb TOA NDUGU.mp3
3.9 Mb Quick_Rocka_Marco_Chali_-_My_Life
marcochali@marcochali.com
7.3 Mb Nikki_Mbishi,_Stereo,_Suma,_One_-_Hisia
Lengo ni kufikisha ujumbe katika hadhira ya kita…
4.3 Mb WE_GO_HARDER_B_’hits_Anthem-Pancho_&_M_x_ft_Mabeste,Leo(Lio),Izzo_Biznes,Young_D,Shettah,Roma,G_zillah,Quik_Rocker_&_E-The_Sniper,Produced_by_PANCHO,mastering_by_Hermy_B.mp3
3.3 Mb GOOD LOOK-AY FEAT. MS. TRINITY.mp3
7.7 Mb GYPTIAN+BANX,G.NAKO-HOLD YA RMX.mp3
Gyption, Banx, G nako – Hold Ya Remix
2011
The Mbele Reality Show Coming Soon by Albino Fulani
Mbele is a docudrama film about the journey of a music artist “Albino Fulani” as he links up with his fellow Tanzanian artist LBT for a USA benefit concert tour (S.A.P – Save Albinos Project). Being an Albino person himself, this show will take you behind the scenes where you will see dramatic episodes on how Albino Fulani associate and interrelate
The benefit concert takes place yearly to help raise funds which help children with albinism in Tanzania and also to raise awareness. The docudrama will show you how the two artists face and overcome professional and personal struggles and obstacles to raise funds and make the benefit concert a success.
The first season consists of 10 episodes which is expected to air in major Television Networks in Tanzania, Kenya and Uganda. Please join and “like” us on our Facebook page http://www.facebook.com/pages/Mbele/128019230601306 where as a member you will receive inside information and you will be able to watch the previews, behind the scene photographs and updates before the public does.
Stay tuned for the official trailer to be released on April 20th 2010. Please join the above facebook page to be the 1st to watch and comment.
Your support is very much needed and appreciated.
Sponsors and media please contact thembeleshow@gmail.com
Thank you.
2011
Hip Hop Ya Tanzania: Ni ubunifu au kubuni tu
Tanzanian Hip Hop — A Culture of Recycling?
Chimbuko la Hip hop linaweza kufafanuliwa kwa kifupi kama ‘juhudi za wasiojiweza’. Hili lilionekana dhahiri wakati Wamarekani weusi walipokuwa wakipigania haki zao za kijamii, wakati huo wa civil rights movement. Hapa kwa haraka tunaona uhusiano wa Hip Hop na jamii. Hip Hop ikiwa upande wa wanyonge, ikitumika kama sauti ya wakandamizwaji.

Miaka hiyo imekwishapita na muziki huu umekua na kuwa ni utamaduni. Lakini bado umebaki na damu ya uanaharakati. Hip Hop imebadilika kama tamaduni yeyote ile, na mpaka kuvuka mipaka. Mipaka hiyo ilivuka hadi kufika Tanzania ambako ilikaribishwa. Boardman anajenga hoja kuwa, Hip Hop ilifanikiwa kuvuka mipaka ya Tanzania kutokana na kuanguka kwa Siasa ya Ujamaa. Mwanzo ulikuwa mgumu, na bado safari ni ndefu, lakini mafanikio yanaonekana; kama kukubalika na jamii.
Muziki huu hata hivyo bado unaonekana kama ni tamaduni ya Kimarekani zaidi, huku kuna baadhi ya watu kwenye jamii zetu ambao wanaona Hip Hop ya nyumbani ‘ina-recycle’ tu yale yanayofanywa na wasanii wa Marekani. Kwenye hilo natumaini kuwa kila mtu atakuwa na mawazo yake, lakini ili kupata jibu lililo karibu na sahihi, ni vizuri kurudi kwenye chimbuko la tamaduni wa muziki huu wa Hip Hop.
Muziki huu ulikuwa unaitwa “muziki wa kufokafoka” kipindi hicho. Nadhani hilo jina halikuwa sahihi, na uliupa mziki huu taswira mbaya. Lakini kwa kuwa ulikuwa ni muziki mpya, inawezekana hatukujua jina gani litakuwa sahihi. Hata hivyo, ukiangalia kwa karibu labda neno kufoka halikukosea sana, kwani kurap ni kama kufoka — lakini neno sahihi la Kiswahili ni kughani.
Muziki huu ulileta mgongano kati ya kizazi chetu na kizazi cha Tabora Jazz kwani muziki huu uliangaliwa kwa tafsiri tofauti. Muziki huu ulionekana ukiwa na hiyo dhana ya kufokafoka, na kawaida ya tamaduni zetu, mtoto hamfokei mzazi. Hivyo inawezekana Hip Hop ikaonekana ni muziki unaochochea uasi dhihi ya tamaduni zetu za ndio mzee. Lakini kwa upande mwingine, hasa ukiangalia katika chimbuko, huu ni muziki wa watu wanaokandamizwa. Hivyo kipindi kile cha akina II Proud na Wapi Tunakwenda, vijana tulikuwa na madukuduku mengi.

Hip Hop ikafanya vile vile kama ilichofanya Marekani kipindi cha miaka ya sitini na sabini — kuwapa wanyonge sauti. Tofauti ilikuwa, huko Marekani iliwapa watu weusi (hasa vijana) sauti dhidi ya ubaguzi wa rangi. Hapa Tanzania, suala halikuwa ubaguzi wa rangi, lakini kupigania haki za vijana, dhidi ya uonevu wa polisi, dhidi ya maisha magumu kwa vijana n.k. Hivyo ni kweli, mwanzoni kwenye hip hop watu walikuwa wanafoka vilivyo, kwani matatizo yalikuwa mengi na hakuna aliyewasilisha matatizo hayo ya vijana, au hata kuyapa nafasi ya kusikilizwa. Hilo linafanana na makundi kama N.W.A. huko Marekani. N.W.A walikuwa wakali, kwani hali halisi yao ilikuwa ni ngumu sana kipindi hicho, ukilinganisha na sasa.
Sasa kama tamaduni nyingine, Hip Hop imekuwa inakwenda na wakati, pamoja na kuwa kwenda na wakati huko hakujasaidia sanaa hii moja kwa moja. Maisha yamebadilika, vijana wa juzi waliokuwa wanapigania haki zao, leo baadhi wamefanikiwa. Hivyo maudhui ya mashairi yamebadilika kwa namna moja au nyingine. Kama marekani, vijana wengi wametajirika kupitia mgongoc wa Hip Hop, hivyo kuanza kughani kuhusu utajiri wao, kwasababu hawaishi tena kwenye ghettos kama awali.
Hapa Tanzania, kwenye nchi masikini, Hip Hop imekuwa bado ikitegemewa katika kutetea haki za wanyonge na kuzungumzia matatizo ambayo yanaendelea kukabili vijana wengi. Pamoja wapo wachache, waliofanikiwa, wengi wa vijana bado wapo kwenye hali ngumu. Hapa ndipo neno “Hali Halisi” linapoingia katika kuchambua Hip Hop ya Tanzania. Wapo ambao wanahesabiwa kama si wana Hip Hop, kwani mashairi yao hayazungumzii hali halisi ya maisha ya kijana wa kila siku wa Kitanzania. Hili linaendana na picha zilizomo kwenye video nyimbo zao. Video nyingi zinaonekana kushindwa kuakisi yaliyomo katika tamaduni zetu, bali huakisi zaidi yaliyomo katika mila na desturi za tamaduni za Magharibi.
Hili suala la mila na desturi ni mjadala mwingine, kwani video hizi huonekana kama zinakiuka maadili ya mila na desturi zetu. Mengi yamezungumzwa, bila kufafanua nini maana ya mila na desturi zetu, kwani kama suala ni mavazi ya uchi, basi kuna Wamasai ambao hutembea wamevaa lubega tu, bila kuwa na mavazi ya ndani. Wapo wengine ambao wanaona picha za kwenye video za Hip Hop zinahamasisha maovu; kwa mfano ngono, kama vile video nyingi za Hip Hop za Marekani. Kama hilo ni tatizo, basi tunaweza kubadilishakituo cha runinga na kuweka mduara, ambao naamini ni tamaduni yetu.
Hata hivyo, kuna machache ambayo wapinzani wa Hip Hop hawajakosea sana.
Sehemu ya pili itafuata…
Hata hivyo, kuna machache ambayo wapinzani wa Hip Hop hawajakosea sana. Moja ni kuchukua utamaduni wa mtu mwingine na kusahau kuainisha — kwa makusudi au bahati mbaya — na hali halisi yako binafsi. Kama jinsi uanaharakati wa muziki huo unapotumiwa na vijana wa Tanzania kupigania haki zao za kijamii ambazo zinatofautiana na zile za vijana wa Marekani (wakati wa civi rights movement). Tatizo ninaloliona hata mimi leo ni hili la kunakili kila kitu cha Magharibi, mpaka kusahau hali halisi ya mazingira yetu yanayotuzunguka.
Kwa mfano, tukiangalia video hii, utaona mambo mengi ambayo yanafanana sana na mambo tunayoyaona kwenye video za Marekani. Hii ndiyo inaweza kutafsiriwa kama “recycling” yenyewe. Wakati kwenye video hii ya pili, pamoja msanii kuchukua baadhi ya mambo ya tamaduni ya Hip Hop ya Marekani, lakini ameweza kuchangaya na mambo yaliyo kwenye tamaduni yake. Hapo unaona utofauti kati ya video ya msanii wa kwanza na msanii wa pili.
Hapa sio kwamba napinga alichofanya msanii wa kwanza, na kuona ni upuuzi mtupu; kwani hii ni sanaa, na sanaa ni ubunifu, na ubunifu huo husaidiwa na fikra. Lakini, hapo ndipo kuna hatari ya Hip Hop ya Tanzania kuonekana kama “ina-recycle” tu yale ya Hip Hop ya Marekani. Pamoja Hip Hop ya msanii wa kwanza bado itaitwa Hip Hop, lakini itakuwa si Hip Hop halisi kwani haiakisi hali halisi ya jamii inayomzunguka.
Ndugu Boardman kwenye makala yake ya Bongo Flava & The Urban Youth Of Tanzania, anaelezea moja kati ya vitu inayotofautisha Hip Hop ya Tanzania na Marekani ni hili la ‘Kiswacentrism’. Yeye anadai kuwa matumizi ya Kiswahili ni moja ya kitu kilichotofautisha Hip Hop ya Tanzania na Marekani, na hilo hata kuanza kuchochea utofauti wa maudhui ya nyimbo za wasanii wa hapa nyumbani. Hili nakubaliana nalo, kwani ni vigumu kuelezea au kuongelea matatizo yako, kwa kutumia lugha ya mtu mwingine. Lakini pamoja matumizi ya Kiswahili yaliipa Hip Hop ya Tanzania kitambbulisho chake, hicho ndicho kitu pekee ambacho kinatofautisha Hip Hop ya Tanzania na Marekani?
Lazima tuendelee kukumbushana kuwa Hip Hop ni tamaduni. Pia ni sanaa hivyo wasanii watakuwa wabunifu, na wapo wale ambao watakuwa wabunifu mpaka watajisahau. Lakini pamoja na hao, wapo wale ambao watakuwa na misimamo yao mikali, na watabaki katika kundi la kughani Hip Hop inayoakisi hali halisi, au kwa maneno mengine, real Hip Hop. Pia, kufokafoka huko kutakuwepo wakati wa kughani, kwani katika hisia za kawaida za mwanadamu, pindi akasirikapo sauti nayo hubadilika. Ni kama kwenye msiba watu hawaendi pale wakigaragara chini kwa kicheko, kwani hisia za kawaida ni hisia za huzuni, kwani hiyo ndiyo hali halisi.
Mwisho, tukubali au tusikubali, tamaduni hii itaendelea kupingwa na wachache, na kuonekana ni uhuni tu, bila ya kutegea masikio tungo zake. Pamoja wapo ambao wataona ni kilele tu na si ushairi, kwani tungo zake hazifanani na tungo za Shaaban Robert. Fikra hizi hazitaondoa ukweli kuwa nyimbo za Hip Hop ni kazi ya sanaa. Maudhui yake yanaweza yasiwe ya kushabikia maovu, au kuwa ya unyenyekevu, bali yenye kuuliza maswali makali kwa wale walio katika nafasi za uongozi au mamlaka, hivyo kuonekana kama ni aina ya muziki unaochochea utovu wa nidhamu.
Uhalisi wa hii sanaa ni lazima ulindwe, au ni kweli Hi Hop ya Tanzania itaonekana ni sanaa “inayo-recycle” tu maisha ya watu wengine, hivyo na muda itapoteza kitambulisho chake.
Kutoka TZHIPHOP.com na imeandikwa na BAHATI MABALA



